TOFAUTI KATI YA MFANYA BIASHARA NA MFANYA KAZI (MTUMISHI WA UMMA)

Kitanzi kipya watumishi wa umma - Mtanzania

Kitu nimechogundua katika safari yangu ya maisha baada ya ku experience vyote viwili kwa muda mrefu, ni kwamba kuna tofauti kubwa ya wasomi hasa watumishi na wafanya biashara. Miongoni mwa tofauti hizo ni

1:Elimu , biashara inahitaji skills na skills una experience while ajira nyingi za bongo zinaangalia vyeti vya knowledge na knowledge una learn .hapa naomba nieleweke vizuri., Elimu pote inahitajika bali elimu itayokusaidia katika biashara ni uzoefu utakaoupata kutokana na shughuli zako za kila siku. Hivyo Elimu zetu za vyeti zinatupa uzito kufanikisha biashara kwasababu hazina mahusiano ya moja kwa moja na uhalisia wa biashara

Kwahiyo hata kama umesomea biashara ila ili uwe mfanya biashara unahitajika ufanye kwanza biashara (u experience) kwa vitendo uachane na utajili wako wa kwenye diary .Biashara ina mambo mengi tofauti na tunavyofundishwa hivyo ili uyajue lazima uwe umewahi kuifanya na sio unakuta mtu hajawahi kuuza hata Karanga afu anajikuta Bakhresa.

2: Ujasiri/ roho ngumu. Biashara inahitaji roho ngumu kupita maelezo. Mfanya biashara suala la kupata na kukosa ni kitu cha kawaida, habari za kupiga hasara, kuzulumiwa na kukata upepo ( mzigo hautoki) ni sehemu ya maisha yake. Mtu yeyote alie kwenye biashara kwa muda mrefu huwa anaujasiri usio kipimo mana anayoyapitia ni zaidi ya vita vya kijeshi. Ila wenzangu na mimi hatuna presha tuna count tarehe tu , kama kipindi hichi najua michomekeo itakuwa mingi mtaani.

3. Biashara inahitaji umakini wa hali ya juu kuliko. Najua kuna kazi nyingi zinahitaji umakini mkubwa katika kuzifanikisha ila biashara ni kiboko. Kuna msemo mzee wangu anapenda kuusema kuwa "akili zunguluka mali potea" yani kibiashara haijalishi biashara kubwa au ndogo ukicheza kidogo tu unahesabu maumivu .kidogo ajira huwa zinatulinda wavivu na wazembe ukikosea unaonywa.

4: Biashara ni upepo. Nikitumia neno "upepo " wafanya biashara wananielewa, yani unaweza kimbiza leo kesho ukabuma, unaweza ukapata losi mwaka huu ila mwakan ukatoboa. Wakati waajiliwa ni mkataba tu ndo unaamua hatima yako.

5.: Biashara inakulazimisha kufikilia baada yakufikilia, kufanya baada ya kufanya. Kila siku uwe na wazo jipya uwe na mtandao mpya na uwe na bidhaa mpya. Hivyo kila ukimaliza kuwaza hili linakuja lingine. Wasomi wengi makazini mkisha saini daftar la mahudhurio tayari umemaliza siku, kuwaza atawaza bossi .

Hii ndo sababu kubwa ya wafanyakazi kuogopa biashara au kufanya bila mafanikio. Ndugu zangu tusijazane ujinga biashara sio kama mnavyozijadili mitandaoni , biashara sio kama mnavyosoma kwenye vitabu , biashara sio kama mnavyoandika kwenye makaratasi laa hasha biashara ni uthubutu , kujiamini na kujitoa . Nisitofasirike vibaya simaanishi waajiliwa hatuwezi biashara ila namaana mitazamo ya wasomi /waajiliwa kuhusu biashara ni ya nadharia ambayo haiyendani na uhalisia.

Tofauti hizi ni kwa uchache tu mwenye zingine aongezee.
Share on Google Plus

About JE UNAFAHAMU

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Comments :

Post a Comment