UTUNZAJI BORA WA VIFARANGA VYA KUKU


chanjo ya vifaranga vya kuku wa kienyeji - YouTube
Leo natamani kutoa elimu juu ya malezi ya vifaranga wa kuku wa kienyeji ili kupata tija. Napenda niwatoe wasiwasi kwa kuwajulisha kuwa haya mafundisho nitakayoyatoa nimeyasomea ( Agricultural science) na pia nimeyafanyia uchunguzi.Natamani yale mafupi sana ila yenye ubora

Kwanza kabisa napenda kutoa elimu ya kutumia mtaji mdogo na matumizi ya mazingira yanayomzunguka mtu ili aone faida yake na akupe mtaji wake kulingana na uwezo na mahitaji yake.

Hatua za kuzingatia ili kulea vifaranga wako vyema ni kama ifuatavyo:
1. Baada ya vifaranga kuangaliwa unapaswa kuandaa mazingira mapya mfano box.

2. Andaa chanzo cha joto mfano chungu weka jivu kisha fukia mkaa unaowaka weka pembeni ya box.

3. Weka tandiko ndani ya box kisha weka pumba laini ndani ya box.

4. Vinyweshe vifaranga glucose au maji yenye glucose asubuhi.

5. Viingize vifaranga kwenye box.

6. Baada ya siku mbili anza kuvipa pumba laini bila maji na badala yake viwekee maziwa fresh na kisha vipe tena maji.

Endelea kufanya hivyo kwa mwezi mmoja kisha nipe mrejesho.Lengo hapa ni kuhakikisha Tembe anaangua vifaranga na kutipoteza muda kulea vifaranga ili atage tena na kuangua tena.Ila hakikisha tembe wako na jogoo wanakula vizuri vyakula vyenye protini, maji, wanga, mafuta ,maji na matunda.
Share on Google Plus

About JE UNAFAHAMU

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Comments :

Post a Comment