Zijue faida na hasara za kuajiriwa

Ajira zaongezeka | East Africa Television


Faida za Ajira:

1. Uhakika wa kipato kwa kila mwezi. Haijalishi hali ya uchumi imepanda au imeshuka, kipato kinabakia palepale.
2. Uhakika wa matibabu kupitia BIMA YA AFYA.
3. Kupata connections mbalimbali za Wadau.
4. Kuwa na uhakika wa kupata MKOPO kwa dhamana ya ajira yako.
5. Kuwa na social capital.

HASARA.
1.Kuwa mtumwa kwa mwajiri (kukosa uhuru wa kuamua wapi uishi, lini usafiri, kazi gani ya ziada ufanye)

2.Kuendelea kuishi maisha fukara maana kwa kawaida mwajiri hulipa mshahara wa mfanyakazi aweze kula na kuvaa na siyo kuendelea kimaisha kwa kumiliki mali. Chunguza Wafanyakazi wengi utapata majawabu.

3.Kuishi maisha yenye stress na hofu wakati wote kwa kuhofia mwajiri wako atasema nini juu yako kwa kesho yako.

4.Kuishi maisha yasiyo na furaha na Amani, haswa Mama na Baba mnapokuwa waajiriwa katika sehemu tofauti.

5. Kuwa mtumwa wa madeni na mikopo. Waajiriwa wengi hukopa kufanya ujasiriamali ili hali hawana nafasi ya kusimamia miradi wanayoianzisha na hivyo kuishia kuwa watumwa wa mikopo na madeni baada ya hasara wanazopata mara kwa mara.

Ni juu yako kuchagua aina ya maisha unayohitaji.!
Share on Google Plus

About JE UNAFAHAMU

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Comments :

Post a Comment