JE WAJU; MAJIBU YA MASWALI HAYA YAWEZA KUPATIKANA KATIKA BIBLIA

(Majibu ya maswali haya yaweza kupatikana katika maandiko ya Biblia ambayo yameonyeshwa, na orodha kamili ya majibu imechapwa kwenye ukurasa wa 27. Kwa habari zaidi, ona kichapo “Insight on the Scriptures,” kilichochapishwa na Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc.)
1. Bahari ya Galilaya iliitwaje pia, jina linalotokana na jiji lililo magharibi mwa ukingo wake? (Yohana 6:1; 21:1)
2. Ni wapi waliposimama wapiganaji wa Daudi 200 kati ya 600 kwa sababu ya kuishiwa nguvu walipokuwa wakiwafuata Waamaleki waliokuwa wamewateka wake wawili wa Daudi? (1 Samweli 30:9, 10)
3. Rahabu alitumia nini kuwaficha wapelelezi wawili wa Israeli? (Yoshua 2:6)
4. Ni nini ambacho Paulo alisema kingewasaidia Wakristo ili ‘waweze kumtolea Mungu katika njia ya kukubalika utumishi mtakatifu’? (Waebrania 12:28)
5. Kulingana na Sheria ya Kimusa, bwana-mkubwa alipaswa kufanya nini ikiwa mtumwa wake hakutaka kuwekwa huru? (Kutoka 21:6)
6. Ni jiji lipi la Edomu lililojulikana kwa hekima yake? (Yeremia 49:7)
7. Milango ya Patakatifu Zaidi pa hekalu la Solomoni ilijengwa kwa mbao zipi? (1 Wafalme 6:31-33)
8. Kulingana na Mithali 6:17-19, ni mambo gani saba anayoyachukia Yehova?
9. Herufi ya mwisho ya alfabeti ya Kiebrania ni ipi? (Zaburi 119:169, NWmaandishi ya utangulizi)
10. Ni nini ambacho Paulo alisema kitatukia kwa wale wanaopanda kwa uhaba, kwa kulinganishwa na wale wanaopanda kwa wingi? (2 Wakorintho 9:6)
11. Alipokuwa akidai kwamba Yehova aondoe baraka zake kutoka kwa Yobu, Shetani alidai Yobu angefanya nini? (Ayubu 1:11)
12. Ni nini kitakacholipata “jina la mtu mwovu”? (Mithali 10:7)
13. Yesu alipowasafisha watu kumi wenye ukoma, ni wangapi kati yao waliokosa kuonyesha shukrani? (Luka 17:17)
14. Waisraeli walifanya nini ndipo kuta za Yeriko zikaanguka? (Yoshua 6:5)
15. Ni vizuizi vipi vilivyowekewa Waisraeli waliotukia kuona kiota cha ndege? (Kumbukumbu la Torati 22:6, 7)
16. Kwa nini Yehova aliwapa Waisraeli pendeleo la pekee? (Isaya 41:8)
17. Ni maakida wangapi waliokuwa washauri wa Mfalme Ahasuero, wakishirikiana katika hukumu dhidi ya Malkia Vashti? (Esta 1:14)
18. Sadaka iliyotolewa kwa Yehova ambayo hakuna sehemu yoyote iliyobakishwa na mwabudu. (Mambo ya Walawi 1:4)
19. Ni mambo gani mawili aliyosema Paulo ambayo mtu apaswa afanye ili aokolewe? (Waroma 10:9)
20. Ilimchukua Solomoni muda gani hivi kulijenga hekalu? (1 Wafalme 6:1, 38)
21. Ni nini kilichofanywa katika siku za zamani ili kummaliza nguvu adui aliyetekwa? (Waamuzi 1:6)
22. Musa aliweka wapi mbao za mawe ya Sheria mara ya kwanza? (Kumbukumbu la Torati 10:1-5)
23. Ni kitabu kipi cha Biblia kinachoeleza kwa msingi utendaji wa Petro na Paulo?
24. Aliitwaje yule msichana-mtumishi, aliyefurahi sana kwa kusikia sauti yake, na aliyekimbia kuwaeleza wengine kwamba Petro alikuwa mlangoni, bila kumfungulia? (Matendo 12:13, 14)
Majibu ya Maswali
1. Bahari ya Tiberiasi
2. Kijito Besori
3. Mabua ya kitani
4. “Hofu ya Kimungu na kicho”
5. ‘Kulitoboa sikio lake kwa uma’
6. Temani
7. Mbao za Mzeituni
8. “Macho ya kiburi, ulimi wa uongo, na mikono imwagayo damu isiyo na hatia; moyo uwazao mawazo mabaya; miguu iliyo myepesi kukimbilia maovu; shahidi wa uongo asemaye uongo; naye apandaye mbegu za fitina kati ya ndugu”
9. Taw
10. Wanavuna kulingana na jinsi walivyopanda
11. Angemkufuru Yehova mbele za uso wake
12. Litaoza
13. Tisa
14. Walipopiga kelele
15. Wangeweza kutwaa makinda lakini, koo alipaswa kuachwa
16. Walikuwa “mzao [“mbegu,” NW] wa Ibrahimu,” rafiki ya Yehova
17. Saba
18. Sadaka ya kuteketezwa
19. Mtu apaswa kutangaza hadharani kwamba Yesu ni Bwana, na kudhihirisha imani kwamba Mungu alimfufua kutoka kwa wafu
20. Miaka saba
21. Vyanda vyake vya mikono na vya miguu vilikatwa
22. Ndani ya sanduku lililotengenezwa kwa mshita
23. Matendo
24. Roda
Share on Google Plus

About Habarimotomoto

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Comments :

Post a Comment