Maajabu ya dunia
Maajabu ya dunia ni orodha ya majengo saba ya pekee iliyojulikana na Wagiriki wa Kale. Wagiriki waliita majengo hayo ΤÀ ΕΠΤÀ ΘΕÁΜΑΤΑ ΤΗΣ ΟΙΚΟΥΜÉΝΗΣ (ΓΗΣ) ta hepta theamata tes oikumenes (ges) - Maajabu saba ya dunia inayokaliwa).
Mara ya kwanza majengo ya ajabu yaliorodheshwa na mwandishi Herodoti mnamo 450 KK. Ilhali maandiko yake hayakuhifadhiwa, habari hii inatokana na waandishi wengine waliomrejea. Kulikuwa na orodha tofauti[1][2] lakini ile inayojulikana na kutajwa zaidi ni ile ya Antipater wa Sidon[3]
Ilhali orodha hii ilikusanywa na waandishi wa Ugiriki ya Kale kuna majengo tu yaliyojulikana katika ustaarabu huo. Kwa hiyo hakuna mifano kutoka Uhindi, China, Asia ya Mashariki, Amerika, Afrika kusini ya Sahara wala Ulaya ya Kaskazini.
Majengo ya orodha ya Antipater hayakudumu hadi leo, isipokuwa Piramidi za Giza. Mengine yaliharibika kutokana na matetemeko ya ardhi au kubomolewa, tena hadi leo hapajulikani mahali pa "Mabustani ya Semiramis". Sanamu na picha za kuchongwa kutoka Kaburi la Mausolo na Hekalu la Artemis zilikusanwa na kuhifadhiwa katika Makumbusho ya Britania mjini London, Uingereza.
Yaliyomo
- 1Maajabu saba ya Kale
- 2Maajabu ya dunia ya sasa
- 3Picha za "Maajabu ya Kisasa"
- 4Tazama pia
- 5Tanbihi
- 6Marejeo
- 7Viungo vya nje
Maajabu saba ya Kale
- Piramidi za Giza (Misri ya Kale)
- Mabustani ya Semiramis (Babeli, leo Irak)
- Hekalu ya Artemis mjini Efeso ((Ugiriki ya Kale, leo Uturuki, Asia Ndogo)
- Sanamu ya Zeus mjini Olympia (Ugiriki ya Kale)
- Kaburi la Mausolo mjini Halikarnassos (Ugiriki ya Kale, leo Uturuki)
- Sanamu ya Kolossos kisiwani Rhodos (Ugiriki ya Kale)
- Mnara wa Pharos ya Aleksandria (Misri)
Kati yake piramidi pekee zimebaki hadi leo.
Maajabu ya dunia ya sasa
Katika ulimwengu kila siku maajabu yanaongezeka na kufanya maajabu mapya ya dunia kukubalika mara kwa mara. Kwa mfano, mwaka 2016 kuna maajabu yake. Orodha ya maajabu hayo hutolewa na watu mbalimbali kwa mitazamo tofautitofauti: wengine wanaishia upande wa majengo, wengine wanahesabu hata mazuri ya uasilia n.k.
Vitu hivi hadi kufikia kuitwa maajabu ya dunia ina maana ni vya pekee duniani kote, na hakuna kitu kingine kama hicho au cha kufanana nacho.
0 Comments :
Post a Comment