Asasi za Kiraia 220
zimefanya uchambuzi wa muswada huo wa sheria na kuwasilisha mapendekezo
ya mabadiliko ya muswada huo kwa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria.
Taasisi hizo zimeeleza kuwa japo kuwa zinafahamu muswada huo una lengo
wa kusasisha Sheria iliyopo sana huku ikibaki kuendana na Katiba, ni
mambo machache sana yanaenda na Katiba ya Tanzania ya Mwaka 1977
Asasi hizo zimesema wakati mambo machache yaliyopendekwa kwenye muswada huo yanaendana na Katiba au yanaifafanua Katiba vema, mambo mengi kwenye muswada huo yanakengeuka na kwenda kinyume na Katiba
Baadhi ya mambo yanayoenda Kinyume na Katiba ni;
Je, una maoni gani kuhusu muswada huu unaotarajiwa kupitishwa Bungeni hivi karibuni?
Asasi hizo zimesema wakati mambo machache yaliyopendekwa kwenye muswada huo yanaendana na Katiba au yanaifafanua Katiba vema, mambo mengi kwenye muswada huo yanakengeuka na kwenda kinyume na Katiba
Baadhi ya mambo yanayoenda Kinyume na Katiba ni;
1. Kifungu cha 7(b)(2) na 7(b)(3) of Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No.3) 2020
Mapendekezo
ya mabadiliko ya sheria yanaruhusu wale tu walioathiriwa moja kwa moja
na uvunjifu fulani wa haki kufungua mashitaka ya kudai haki zao.
Mabadiliko haya yakipitishwa yatazuia raia wengine kufungua mashtaka kwa
maslahi ya umma wanapohisi kuna uvunjifu wa Katiba.
Kwa
maana nyingine, hutaruhisiwa kumtetea raia mwenzako hata kama hana
uwezo wa kujitetea, hutaruhisiwa kutetea nchi yako kupitia Mahakama
isipokuwa pale tu unapokuwa umenyanyaswa moja kwa moja, na hutaweza
kutoa mchango wako kuilinda Katiba yetu. Hii inaondoa uzalendo.
>>> Mapendekezo
hayo yakiwa hivyo, Ibara 26 ya Katiba inampa kila raia jukumu na uhuru
wa kuilinda Katiba yetu kupitia Mahakama ya nchi.
Athari kwenye maisha ya kila siku:
Kwenye maisha ya kila siku tulio wengi tunakutana na changamoto za hapa
na pale. Kuna mifumo tofauti kutusaidia kukabiliana na hizi changamoto
ikiwemo, kwa matatizo makubwa na magumu, mifumo ya Mahakama.
Kutoruhusu
mtu au taasisi kufungua mashtaka bila kuathirika moja kwa moja
inakulazimisha kujitegemea na kujitetea unapokutwa na unyimwaji wa haki
zako unaohitaji Mahakama kuingilia.
Kuna
watu wengi ambao wamesaidiwa kudai haki zao na mashirika tofauti ambao
wanawasaidia kwa utalaamu, rasilimali na mikakati na kusimamia kwa
ujumla mashtaka yao. Mabadiliko haya yatawaathiri sana wasiokuwa na
uwezo na ujasiri wa kujisimamia wenyewe kisheria kama vile walemavu,
watoto, wajane na makundi mengine mengi ya kijamii ambayo yamekuwa
yakisaidiwa na watetezi wa haki za binadamu kwa maslahi ya Umma.
2. Kifungu cha 7(b)(4) na 18A na 65A of Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No.3) 2020
Mabadiliko
ya sheria yanaondoa maana ya kuwa Jamhuri na badala yake tunaanza
kulekea kwenye utawala usiokuwa wa kisheria kama vile utawala wa
kifalme. Kwenye Jamhuri watu wote, wananchi na viongozi, wanaangaliwa
sawa kwa jicho la sheria. Ndio tunaoita utawala wa sheria – kila mtu awe
mdogo au mkubwa, anawajibika kwa kile alichofanya mwenyewe.
Kwa
kuwatoa watu fulani kutoka mfumo wa kawaida wa haki, mfumo wa Mahakama,
na kufanya hawawezi kuwajibishwa moja kwa moja, hata kama wamekiuka
Katiba, inatupeleka kuwa na ngazi mbili za raia, wanaofuata sheria na
wasiofuata sheria.
Pamoja
na haya, misingi ya demokrasia na Jamhuri yetu ni mihimili mitatu ya
Serikali, Bunge na Mahakama. Kila mhimili una majukumu yake na haitakiwi
kabisa kuingiliana.
Mhimili
mmoja unawajibisha mwingine kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo na
haki. Hii haijalishi nani anashika cheo cha Rais, ni msingi wa Katiba
yetu, nchi yetu na sheria zote za nchi.
>>>
Ibara ya 13 ya Katiba inaeleza usawa mbele ya sheria kwa kila mwananchi
na Ibara ya 4 inazungumzia mihimili mitatu ya Serikali na jinsi
zinavyotakiwa kushirikiana, kila taasisi kwa uhuru wake.
Athari
kwenye maisha ya kila siku: Kuna watu wanaopenda kusema demokrasia siyo
chakula. Ukweli ni kwamba haki za mfumo wetu wa utawala, zinajulikana
kama haki za siasa, hazionekani wazi kwenye maisha ya kila siku kama
ilivyo kwa haki nyingine kama za kuishi na kupata chakula.
Tunaporuhusu
baadhi ya watu kuwa nje ya sheria ambazo sisi wote tunazifuata,
tunatengeneza mazingira tatanishi ya kutegemea utashi mtu moja au watu
wachache. Wao ndio wataamua utamu na ugumu wa maisha yetu bila sisi kuwa
na mchango wowote.
Mamlaka
ya viongozi wetu wote yanatoka kwa wananchi na kila hatua inayotupeleka
mbali na hilo, inazidi kupunguza uwezo wetu wa kuamua mwelekeo ya
maisha zetu.
3. Kifungu cha 7(b)(2) na 7(b)(3) na 18A na 65A of Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No.3) 2020
Haya
mabadiliko ya sheria yanawapa kundi la watu Mamlaka juu ya sheria na
yanapunguza uwezo wa baadhi ya watu kudai haki nchini. Kwa sababu
Mahakama ni sehemu ya mwisho kupeleka kilio chako ukinyimwa haki, hii ni
sawa na kutomruhusu mtoto kulia unapompiga.
Tunahitaji
kutoa dukuduku letu na kuamini kwamba tunapokanyagwa na mtu yoyote,
tutafidiwa. Utawala wa sheria unategemea imani yetu katika mifumo ya
sheria. Mifumo yetu ya sheria ikianza kuleta ubaguzi kuanzia kwenye
sheria zenyewe ndio tunaelekea kuuua mfumo yenyewe.
>>> Ibara 26 ya Katiba inampa kila raia jukumu na uhuru wa kuilinda Katiba yetu kupitia Mahakama ya nchi
Athari kwenye maisha ya kila siku:
Tunapofunga milango ya mfumo wa haki nchini ndio walalahoi wanakosa
njia muhimu ya kufidiwa. Watu maarufu na wenye mahusiano na vigogo na
wanasiasa wanaweza kuwa na njia tofauti lakini wananchi wa kawaida
wanategemea mfumo wa Mahakama wanapodai haki zao. Wapi tupeleke kilio
chetu haki zetu zikikiukwa?
Je, una maoni gani kuhusu muswada huu unaotarajiwa kupitishwa Bungeni hivi karibuni?
About JE UNAFAHAMU

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 Comments :
Post a Comment